Uboreshaji wa shughuli za uchimbaji mdogo wa madini nchini Tanzania kupitia ubia na wawekezaji: Fursa na changamoto

Download options
Download document

Ujumbe muhimu

  • Wawekezaji wa kigeni wanazidi kuingia ubia na wachimbaji wadogo ili kupata miliki na hifadhi za madini zilizopo kwenye mazingira hatarishi na yenye gharama kubwa.
  • Hii imechangia ukuaji wa shughuli za wachimbaji wadogo na kusambaza teknolojia katika maeneo yao ya uchimbaji. Hata hivyo ukuaji huu unaweza kuvuruga mpangilio wa ugawanaji faida uliopo kati ya wachimbaji wadogo na wamiliki wa mashimo/leseni.
  • Ukuaji wa uchimbaji mdogo unaotokana na ongezeko la mtaji na usambaaji wa teknolojia umeambatana na hatarishi mbalimbali za kimazingira na usalama na afya kazini.
  • Uwezo mdogo wa taasisi za serikali za ngazi ya chini na ukosefu wa uratibu baina ya taasisi umechangia kudhorotesha juhudi za serikali katika kufuatilia na kuboresha usalama na afya kazini na mazingira katika migodi iliyo chini ya ubia.
  • Kuna umuhimu wa kuwepo kwa majadiliano ya kisera ya haraka juu ya faida na athari za ubia na jinsi ya kuwezesha ubia huu ili kuboresha sekta ya madini na kuleta maendeleo endelevu katika jamii za uchimbaji vijijini.
  • Uratibu wenye ufanisi katika taasisi muhimu za serikali unahitajika kwa haraka, hasa kwenye ngazi ya chini, ili kukabiliana na athari katika mazingira na usalama wa Wafanyakazi zinazotokana na migodi midogo yenye shughuli za kisasa za uchimbaji.
Authors: Schoneveld, G.C.; Chacha, M.; Njau, M.; Weng, X.; Jonsson, J.
Subjects: mining, artisanal method, traditional processing, small businesses, investment, partnerships
Publication type: Brief, Publication
Year: 2018

Back to top

Sign up to our monthly newsletter

Connect with us